Ujana ni hatua ambayo mtu anafikia na kuanza kupevuka kiakili na kutokufikiria vile ambavyo alikuwa anafikiria kipindi akiwa na umri wa kitoto hapa unatakiwa aanzae kujitegema katika kufikri na kuweza hata kuwasaidia wengine.
Kijana ni suala la mtu kujinasibu kwa ujana ni suala la umri pekee. Kwamba mimi nina miaka 25 basi miaka hii ni kigezo tosha cha kuwa kijana.Naweza kukuambia ya kwamba ujana sio umri tu bali ni zaidi ya umri. Mimi nimekuwa nikijiuliza je, kwa mazingira yetu(tz) vijana ni akina nani? Je, ni wale wanaojitahidi kufikiri kwa mantiki na kutoa majawabu kwa baadhi ya matatizo yanayozunguka jamii au ni wale waliogeuka vidaka tonge kwa kukubali kutumiwa na waovu wenye uchu na mali iwe katika siasa, madhehebu ya dini, n.k.Je, ujana ni kuwa na msimamo wenye kuogozwa na hoja zenye mashiko na uthubutu katika kuchochea maendeleo ya jamii au ni kujisalimisha kwa waovu na kuwatetea kwa nguvu zote katika harakati zao (kisiasa,kiuchumi n.k) na kutegemea kuambulia makombo. Je, vijana tunafikiri au haki yetu ya kufikiri tumeirasimisha kwa wengine (wenye uwezo na umaarufu). NAOMBA TUTAFAKARI PAMOJA.