Ujana nini? Na Kijana ni nani?

Ujana ni hatua ambayo mtu anafikia na kuanza kupevuka kiakili na kutokufikiria vile ambavyo alikuwa anafikiria kipindi akiwa na umri wa kitoto hapa unatakiwa aanzae kujitegema katika kufikri na kuweza hata kuwasaidia wengine.

Kijana ni suala la mtu kujinasibu kwa ujana ni suala la umri pekee. Kwamba mimi nina miaka 25 basi miaka hii ni kigezo tosha cha kuwa kijana.Naweza kukuambia ya kwamba ujana sio umri tu bali ni zaidi ya umri. Mimi nimekuwa nikijiuliza je, kwa mazingira yetu(tz) vijana ni akina nani? Je, ni wale wanaojitahidi kufikiri kwa mantiki na kutoa majawabu kwa baadhi ya matatizo yanayozunguka jamii au ni wale waliogeuka vidaka tonge kwa kukubali kutumiwa na waovu wenye uchu na mali iwe katika siasa, madhehebu ya dini, n.k.Je, ujana ni kuwa na msimamo wenye kuogozwa na hoja zenye mashiko na uthubutu katika kuchochea maendeleo ya jamii au ni kujisalimisha kwa waovu na kuwatetea kwa nguvu zote katika harakati zao (kisiasa,kiuchumi n.k) na kutegemea kuambulia makombo. Je, vijana tunafikiri au haki yetu ya kufikiri tumeirasimisha kwa wengine (wenye uwezo na umaarufu). NAOMBA TUTAFAKARI PAMOJA.

Unatambua ya kuwa wewe ni mbeba maono

Kwa wale wasomaji wa biblia tunaona ya kuwa Yusuph alikuwa anaweza kutafsri ndoto za watu je wewe unaweza kama kijana?. Kama kijana unaweza kujiuliza ndani yako umebeba nini? Je unajua thamani yako kama kijana?je rafiki uliyenaya ana ndoto kama za kwako. Hayo ni maswali ya kijiuliza kama kijana na pia unatakiwa ujue kuwa sio kila ndoto unayoota unapaswa kuisema zingine ni siri.

Dhumuni la wewe kuwepo duniani

Ni lazima ujue wewe ni kwanini ulikuja duniani kama binadamu  wala sio ng’ombe, mbuzi ,samba au hata mnyama au mdudu mwingine yoyote ni kwa sababu kuna kusudio Mungu aliloliweka ndani yako na ni lazima ulijue na ulifanyie kazi kwa wakati unaostahili kwamaana ukilojua tu alafu haulifanyii kazi haitakusaidia chochote na vizuri ukajua mapema na ukaweza kufanya mambo makubwa zaidi hata jamii ikashangazwa na ulichokifanya kusudio ni ujue nini kimekuleta duniani.

Kumjua Mungu

Bila kumjua Mungu hautaweza kufanikiwa  katika kiimani na pia kimwili bila kuangalia dini au imani yako watu wote wanamuhitaji Mungu katika maisha yako kwa hiyo basi unatakiwa ujitahidi walaukila mara uwe unamwabudu Mungu wako sababu yeye ndio kila ktu chukulia mfano kama tungekuwa tunaendesha maisha yetu wenyewe tungelikuwa wapi hivi leo kama sio tungekwishakufa  jamani tumtafute sana Mungu wetu.